TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI
Katibu wa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma kwa niaba ya Mamlaka ya Hifadhi za Taifa (TANAPA) anapenda kuwataarifu waombaji kazi wote walioomba kazi zilizotangazwa kwa niaba ya Mamlaka hiyo kuwa usaili unatarajiwa kuendeshwa kuanzia tarehe 25 - 29 Januari, 2022 katika Kambi ya Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) Oljoro Arusha na hatimaye kuwapangia vituo vya kazi waombaji kazi watakaofaulu usaili.
Wasailiwa wanaoitwa kwenye usaili wanapaswa kuzingatia maelekezo yafuatayo:-
i. Usaili utafanyika tarehe 25-29 Januari, 2022 katika Kambi ya Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) Oljoro Arusha kama ilivyooneshwa kwenye tangazo hili; muda na tarehe ambapo usaili utafanyika umeainishwa kwa kila msailiwa;
ii. Wasailiwa wote wanapaswa kuripoti katika Kambi ya Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) Oljoro Arusha tarehe 24 Januari, 2022 ambapo huduma zote za chakula na malazi watapatiwa bila malipo wakiwa kambini;
iii. Usaili wa Vitendo utafanyika kuanzia tarehe 25-27 Januari, 2022;
iv. Usaili wa Mahojiano ya ana kwa ana utafanyika tarehe 29 Januari, 2022;
v. Kila msailiwa anatakiwa kufika kwenye eneo la usaili akiwa amevaa barakoa, kunawa mikono kwa sabuni na maji tiririka ama kutakasa mikono;
vi. Kila msailiwa anapaswa kuwa na kitambulisho kwa ajili ya utambuzi; vitambulisho vinavyokubalika ni pamoja na:- Kitambulisho cha Mkazi, Kitambulisho cha Mpiga kura, Kitambulisho cha kazi, Kitambulisho cha Uraia au Hati ya kusafiria;
vii. Wasailiwa wanatakiwa kufika na VYETI VYAO HALISI, kuanzia cheti cha kuzaliwa, kidato cha IV, VI, Stashahada, Stashahada ya Juu, Shahada na kuendelea kutegemeana na sifa za Mwombaji;
viii. Wasailiwa watakaowasilisha “Testimonials”, “Provisional Results”, “Statement of results”, hati za matokeo za kidato cha IV na VI (form V and form VI results slips) HAVITAKUBALIWA NA HAWATARUHUSIWA KUENDELEA NA USAILI;
ix. Kila Msailiwa azingatie tarehe, muda na mahali alipopangiwa kufanyia usaili;
x. Kwa waombaji waliosoma nje ya Tanzania wahakikishe Vyeti vyao vimehakikiwa na kuidhinishwa na Mamlaka husika (kama TCU, NACTE au NECTA);
xi. Waombaji kazi ambao majina yao hayakuonekana katika tangazo hili watambue kuwa hawakukidhi vigezo. Hivyo, wasisite kuomba tena pindi nafasi za kazi zitakapotangazwa na kuzingatia mahitaji ya tangazo husika.
xii. Wasailiwa wote walioitwa kwenye usaili wahakikishe wanaingia kwenye akaunti zao na kunakili namba ya mtihani kwa kuwa namba hizo
hazitatolewa siku ya usaili.
BOFYA HAPA KUSOMA KWA UKAMILIFU TANGAZO HILI RASMI KUTOKA UTUMISHI