TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kibondo anakaribisha maombi ya Kazi kwa nafasi zifuatazo.
1.0. MTENDAJI WA KIJIJI DARAJA LA III- NAFASI 01
1.1. SIFA ZA MWOMBAJI
Mwombaji anatakiwa awe na cheti cha kufaulu Kidato cha Nne na waliohitimu mafunzo ya Cheti (Astashahada) katika fani zifuatazo: Utawala, Uongozi na Usimamizi wa Fedha, Sheria, Elimu ya Jamii, Maendeleo ya Jamii na Sayansi ya Sanaa kutoka Chuo cha Serikali za Mitaa Hombolo au Chuo/Taasisi yoyote inayotambuliwa na Serikali.
1.2. KAZI NA MAJUKUMU
• Kuandaa taarifa za Utekelezaji wa kazi katika eneo lake na kuhamasisha wananchi katika kuandaa na kutekeleza mikakati ya kuondoa njaa, umasikini na kuongeza uzalishaji mali.
• Kusimamia, kukusanya na kuhifadhi kumbukumbu zote na nyaraka za Kijijj.
• Kiongozi wa wataalamu (watumishi wa serikali) katika kijiji.
• Mhasibu (Afisa masuuli) na Mtendaji Mkuu wa kazi
za kila siku za Serikali ya Kijiji.
• Kutafsiri na kusimamia utekelezaji wa Sera, Sheria na Taratibu zinazotolewa
na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
• Kusimamia Ulinzi na Usalama wa raia na mali zao, kuwa Mlinzi wa Amani na
Msimamizi wa utawala bora katika kijiji.
• Katibu wa Mikutano na Kamati zote za Halmashauri ya Kijjjj.
• Kuratibu na kusimamia upangaji na utekelezaji wa Mipango ya Maendeleo ya Kijii.
• Kutekeleza Shughuli nyingine atakazopangiwa na Mwajiri.
• Atawajibika kwa Mtendaji wa Kata.
1.3. MSHAHARA
Kwa kuzingatia viwango vya Serikali yaani ngazi ya Mshahara TGS B
2.0. KATIBU MUHTASI Ill - NAFASI 01
2.1. SIFA ZA MWOMBAJI
Mwombaji anatakiwa awe na cheti cha kufaulu Kidato cha Nne na waliohudhulia Mafunzo ya Uhazili na kufaulu mtihani wa Hatua ya Tatu. wawe wamefaulu somo la Hatimkato ya Kiswahili na Kingereza maneno 80 kwa dakika moja na wawe wamepata mafunzo ya kompyuta kutoka chuo chochote kinachotambuliwa na Serikali nakupata cheti katika programu za windows, Microsoft office, Internet, Email na Publisher.
2.2. KAZI NA MAJUKUMU
• Kuchapa barua, taarifa na nyaraka za kawaida.
• Kusaidia kupokea wageni na kuwasaili shida zao, nakuwaelekeza sehemu wanapoweza kushughulikiwa.
• Kusaidia kutunza taarifa/kumbukumbu za matukio, miadi, wageni, tarehe za vikao, safari za Mkuu wake na ratiba za kazi nyingine zilizopangwa kutekelezwa katika Ofisi anamofanyia kazi, na kumuarifu Mkuu wake kwa wakati unaohitajika,
• Kusaidia kutafuta na kumpatia Mkuu wake majalada, nyaraka au kitu chochote kinachohitajika katika shughuli za hapo ofisini.
• Kusaidia kufikisha maelekezo ya Mkuu wake wa kazi kwa wasaidizi wake na pia
kumuarifu kuhusu tarifa zozote anazokuwa amepewa na wasaidizi hao.
• Kusaidia kupokea majalada, kuyagawa kwa Maofisa walio katika sehemu alipo, na kuyakusanya, uyatunza na kuyarudisha sehemu zinazohusika.
• .Kutekeleza kazi zozote atakazokuwa atakazokuwa amepangiwa na Msimamizi wake wa kazi
Kibondo, SL.P 43, Kibondo- Kigoma, Simu: +25528-2820084, Nukustr +25528-2820084, Barua pepe: ded@ibondodc.gp.{z Tovuti: www kibondodc.go.t2
[Barua zote ziandikwe kwa Mkurugenzi Mtendaji (W)]
2.3. MSHAHARA
Kwa kuzingatia viwango vya Serikali yaani ngazi ya Mshahara TGS B
2.4. MASHARTI YA JUMLA KWA WAOMBAJI
• Waombaji wote wawe ni Raia wa Tanzania na wenye umri usiozidi miaka 45
• Waombaji wote waambatanishe cheti cha kuzaliwa.
• Waombajj waambatishe maelezo binafsi yanayojitosheleza (Detailed CV yenye anwani na namba za simu za kuaminika pamoja na majina y wadhamini (referees) watatu wa kuaminika.
• Maombi yote yaambatane na vyeti vya taaluma, nakala za vyeti vy Kidato cha Nne na Kidato cha Sita kwa wale waliofikia kiwango hicho n vyeti vya kuhitimu mafunzo mbalimbali kwa kuzingatia sifa za kazi husika.
• Picha moja "Passport size" ya hivi karibuni iandikwe jina kwa nyuma.
• Testmonials", "Provisional Results", "Statement of results", Hati za Matoke ya Kidato cha NNE na RESULTS SLIPS HAVITAKUBAULIWA.
• Maombi yanaweza kuandikwa kwa Lugha ya Kiswahili fasaha au Kingerez fasaha.
• Mwisho wa kupokea barua za maombi ni tarehe 20, Januari, 2022 saa 9:30 Alasiri na yatumwe kupitia Posta kwa anuani ifuatayo:
MKURUGENZI MTENDAJI,
HALMASHAURI YA WILAYA YA KIBONDO, S.L.P 43,
KIBONDO
IMETOLEWA NA:
Rutema D.M MKURUGENZI MTENDAJI (W) KIBONDO
Also See: Other Government Jobs Here
Check Out Other Office Administration Jobs Here
Also View: Other Jobs in Kigoma Here