SHULE INATANGAZA NAFASI YA KAZI YA MPISHI WA KIUME
Description
Shule ya Sekondari ya Arusha Science iliyopo katika Kijiji cha Laroi, karibu na Oljoro JKT inahitaji mpishi mwanamme
KAZI NA MAJUKUMU:
1) Kupikia wanafunzi Pamoja na Walimu, awe nauwezo wa kupikia watu zaidi ya 200
2) Kupikia Wageni wa shule kama wakijitokeza na kama atakavyoagizwa
3) Atamsaida Mpishi Mkuu maswala yote ya jikoni, pamoja na kutengeneza menu ya shule na kuandika mahitaji yote ya jikoni kila wiki
4) Kuripoti tatizo lolote litakalotokea kwenye sehemu yake ya kazi kwa Mkuu wa Kitengo au Mkuu wa shule au Matroni
5) Atashiriki katika utunzaji wa bustani ya mboga mboga ya shule na kuhakikisha mboga zote zilizokomaa zinatumiwa kwa wakati bila kuharibika
6) Kushiriki katika usafi wa jiko na mazingira yanayolizunguka jiko
SIFA ZA MUOMBAJI
- Awe amemaliza kidato cha nne
- Awe amefanya kazi ya kupika katika shule ya Sekondari kwa muda usiopungua miaka miwili
- Awe anajua hesabu na vipimo vya chakula
- Awe anajua kupika vizuri
- Awe anajua kuandaa bajeti
- Awe na nidhamu kwenye kazi na lugha nzuri
- Awe anatambua suala la usafi na ajue kuzingatia muda
- Awe mbunifu katika upishi na uwezo wa kujifunza kutoka kwa wengine