TANGAZO LA KAZI YA MHASIBU
SIFA NA UJUZI
Awe na digrii katika mambo ya Fedha, Benki, Uhasibu au inayolingana na hizo kutoka katikachuo kinachotambulikana.
Awe na sifa za kitaaluma. (CPA, ACCA au inayolingana na hizo) na uzoefu usiopungua miaka mitatu katika mazingira ya biashara ushindani
Mwenye uwezo wa kufanya kazi bila ya usimamizi wa karibu na uwelewa mzuri, mwaminifu na tabia nzuri na uzoefu wa mifumo ya Tehama ya kihasibu ya SACCOS
Recommended for you: Get the Latest & New Job Updates Here
KAZI NA MAJUKUMU
- Kuhakikisha mapato na matumizi yameingizwa katika vitabu vya hesabu kwa
usahihi..
- Kuhakikisha taarifa zote za mikopo, akiba, hisa na amana za wanachama
zimeingizwa kwa usahihi kwenye leja za wanachama
- Kuhakikisha malinganisha ya miamala ya benki na fedha taslimu yanafanyika kila mwezi.
- Kuhakikisha marejesho ya mikopo yanafanyika kila mwezi kulingana na jedwali la marejesho.ya kila mwanachama aliyekopa.
- Kuhakikisha balansi za hisa, akiba, amana na mikopo ya wanachama inalingana na
leja kuu.
- Kutoataarifa ya hali ya mikopo, akiba na amana za wanachama kila mwezi.
- Kutunza daftari la kumbukumbu za wanachama kwa usahihi (members register)
- Kutoa taarifa ya mikopo mibaya kila mwezi.
- Kutayarisha taarifa ya Urari wa hesabu kila mwezi
- Kutayarisha taarifa ya mapato na matumizi kila mwezi.
- Kutayarisha taarifa ya mizania kila mwezi.
- Kutayarisha taarifa ya malinganisho ya bajeti na hali halisi kila mwezi.
- Kutayarisha taarifa ya badiliko la mtaji kila mwezi.
- Kuandaa taarifa ya mtiriko wa fedha kila mwezi, daftari la mali za kudumu na
mishahara ya wafanyakazi.
JINSI YA KUTUMA MAOMBI
• Tarehe ya mwisho ya kupokea maombi 11.02.2022 Saa 10:30 jioni.
Tuma maombi kwa barua pepe kupitia msaccos@mwananchi.co.tz
CV pamoja na vyeti