Katibu wa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma kwa niaba ya Wizara ya Fedha na Mipango, anapenda kuwataarifu Waombaji Kazi wote walioomba kazi za Wizara hiyo kuwa usaili unatarajiwa kuendeshwa kuanzia tarehe 05 - 08 Februari, 2022 na hatimaye kuwapangia vituo vya kazi waombaji kazi watakaofaulu usaili huo. Wasailiwa wanaoitwa kwenye usaili wanapaswa kuzingatia maelekezo yafuatayo:-

TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI


Katibu wa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma kwa niaba ya Wizara ya Fedha na Mipango, anapenda kuwataarifu Waombaji Kazi wote walioomba kazi za Wizara hiyo kuwa usaili unatarajiwa kuendeshwa kuanzia tarehe 05 - 08 Februari, 2022 na hatimaye kuwapangia vituo vya kazi waombaji kazi watakaofaulu usaili huo. Wasailiwa wanaoitwa kwenye usaili wanapaswa kuzingatia maelekezo yafuatayo:-

i.      Usaili utafanyika  kuanzia tarehe 05 - 08 Februari, 2022 kama ilivyooneshwa kwenye tangazo hili;  muda na sehemu ambapo usaili utafanyika umeainishwa katika jedwali la ratiba;
ii.     Kila  msailiwa  anatakiwa  kufika  kwenye  eneo  la  usaili  akiwa  amevaa Barakoa (Mask);

iii.    Kila Msailiwa anapaswa kuwa na kitambulisho kwa ajili ya utambuzi;

iv.  Vitambulisho vinavyokubalika ni pamoja na:- Kitambulisho cha Mkazi, Kitambulisho cha Mpiga kura, Kitambulisho cha kazi, Kitambulisho cha Uraia au Hati ya kusafiria;
v.     Wasailiwa wanatakiwa kufika na VYETI VYAO HALISI, kuanzia cheti cha kuzaliwa, kidato cha IV, VI, Stashahada, Stashahada ya Juu, Shahada na
kuendelea kutegemeana na sifa za Mwombaji;

Dont Miss Out: Get the Latest & New Job Updates Here  

vi. Wasailiwa  watakaowasilisha“Testimonials”,  “Provisional  Results”, “Statement of results”, hati za matokeo za kidato cha IV na VI (form V and form VI results slips) HAVITAKUBALIWA NA HAWATARUHUSIWA KUENDELEA NA USAILI;
vii.   Kila msailiwa atajigharamia kwa chakula, usafiri na malazi;

viii.  Kila Msailiwa azingatie tarehe, muda na mahali alipopangiwa kufanyia usaili;

ix.    Kwa waombaji      waliosoma    nje   ya   Tanzania   wahakikishe   Vyeti   vyao vimehakikiwa na kuidhinishwa na Mamlaka husika (kama TCU, NACTE au NECTA);
x.     Waombaji   kazi   ambao   majina   yao   hayakuonekana   katika   tangazo   hili watambue kuwa hawakukidhi vigezo.  Hivyo, wasisite kuomba tena pindi nafasi za kazi zitakapotangazwa na kuzingatia mahitaji ya tangazo husika.


xi.   Kwa kada ambazo wanatakiwa kusajiliwa na Bodi zao za Kitaaluma wanapaswa kuja na vyeti vyao Halisi vya Usajili pamoja na Leseni za kufanyia kazi.
xii.   Wasailiwa wote walioitwa kwenye usaili wahakikishe wanaingia kwenye akaunti  zao  na  kunakili  namba  ya  mtihani  kwa  kuwa  namba  hizo
hazitatolewa siku ya usaili.

BOFYA HAPA KUSOMA TANGAZO RASMI LIKIWA PAMOJA NA MAJINA.

Recommended for you: Get the Latest & New Job Updates Here