Ticker

Welcome

Tangazo la Nafasi 3 za Kazi / Ajira za Kudumu - Kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Uvinza

 


YAH:  TANGAZO  LA NAFASI  ZA KAZI  Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya  ya Uvinza  anapenda kuwatangazia Watanzania wote kuwa Ofisi imepokea kibali cha Ajira Mbadala kutoka   kwa   Katibu   Mkuu   UTUMISHI   chenye   Kumb.   Na. FA.170/358/01C/91  ya tarehe  26 Novemba, 2021  iliyopokelewa tarehe 24/12/2021  kwa ajili  ya kutangaza  nafasi  ya Mtendaji  wa  Kijiji  III kwa masharti ya  kudumu.  Hivyo Watanzania wote wenye sifa  mnaombwa kuomba nafasi  hiyo kama ifuatavyo:-

 YAH:  TANGAZO  LA NAFASI  ZA KAZI

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya  ya Uvinza  anapenda kuwatangazia Watanzania wote kuwa Ofisi imepokea kibali cha Ajira Mbadala kutoka   kwa   Katibu   Mkuu   UTUMISHI   chenye   Kumb.   Na. FA.170/358/01C/91  ya tarehe  26 Novemba, 2021  iliyopokelewa tarehe 24/12/2021  kwa ajili  ya kutangaza  nafasi  ya Mtendaji  wa  Kijiji  III kwa masharti ya  kudumu.  Hivyo Watanzania wote wenye sifa  mnaombwa kuomba nafasi  hiyo kama ifuatavyo:-


1.  MTENDAJI  WA KIJIJI  DARAJA   LA III (VILLAGE  EXECUTIVE  III).
NAFASI TATU (3)


i)       Sifa za kitaaluma kwa Mwombaji
Kuajiliwa  mwenye  kidato  cha  Nne   (IV)  au  Sita  (VI)  waliopata mafunzo katika  ngazi  ya  cheti  (NTA LEVEL  5) ambao wamehitimu mafunzo ya Astashada/Cheti  katika  moja ya fani zifuatazo.


•   Utawala,  Sheria, Elimu ya Jamii,  Usimamizi  wa fedha,  Maendeleo  ya jamii na Sayansi ya Sanaa kutoka Chuo cha Selikari za Mitaa Hombolo Dodoma au Chuo chochote kinachotambuliwa  na Serikali.

ii)     Majukumu ya kufanya:
-    Afisa Masuhuli na Mtendaji  Mkuu wa Serikali ya Kijiji
Kusimamia Ulinzi  na Usalama  wa raia na mali  zao, kuwa Mlinzi wa amani na msimamizi wa Utawala  Bora katika  Kijiji.
Kuratibu  na kusimamia  upangaji  na utekelezaji  wa  Mipango  ya Maendeleo ya Kijiji  .
Katibu wa mikutano wa Kamati zote Halmashauri ya Kijiji. Kutafsiri  na kusimamia Sera Sheria  na Taratibu.

-   Kuandaa  taarifa za  utekelezaji wa  kazi katika eneo lake na kuhamasisha  katika kuandaa   na  kutekeleza mikakati ya  kuondoa njaa  Umaskini  na kuongeza  uzalishaji  mali.
-    Kiongozi wa Wakuu wa Vitengo vya kitaaluma  katika Kijiji
-    Kusimamia    kukusanya na   kuhifadhi   kumbukumbu    zote  na nyaraka    za  Kijiji,  Mwenyekiti  wa  kikao cha Wataalamu  waliopo katika  Kijiji.
-    Kupokea,   kusikiliza  na kutatua malalamiko  ya Wananchi.
-    Kusimamia   utungaji wa Sheria  ndogo  za Kijiji  na
-    Atawajibika  kwa Mtendaji wa Kata.

iii)     Masharti ya Ajira. Ajira ya kudumu.


iv)     Ngazi ya Mshahara
Ngazi ya Mshahara  wa kuanzia  ni TGS B,




NB:-  Ni  muhimu  kuambatisha  nakala ya kitambulisho cha NIDA au namba ya NIDA katika maombi yako.


Mwisho wa kupokea  maombi  ni tarehe 18 Januari, 2022 Saa 9.30 alasiri


Maombi yote yatumwe kwa:


MKURUGENZI MTENDAJI, HALMASHAURI YA WILAYA, S.L.P 12, UVINZA.


Pakua Hapa Tangazo hili Rasmi Kutoka Tovuti ya Utumishi

 
Also See: Other Government Jobs Here