TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa anayo furaha kutangaza nafasi 04 za ajira ya kudumu kwa watanzania wote wenye sifa stahiki ikiwemo Katibu Mahsusl Daraja la IlI. Mtendaji wa Vljiji Daraja IlI na Dereva Daraja II. Nafasi za ajira hizi zinatokana na Kibali cha ajira mbadala kutoka kwa Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala bora kwa barua Kumb Namba FA.170/372/01'A'/91 ya tarehe 26 Novemba, 2021.
1. MTENDAJI WA KIJIJI III- Nafasi 02
1.1 Kazi Na Majukumu.
• Kuratibu na kusimamia upangaji na utekelezajj wa mipango ya Maendeleo ya Kijiji.
• Kusimamia ulinzi na usalama wa raia na mali zao.
• Kukusanya mapato ya Halamshauri ya Kijiji.
• Kusimamia. kukusanya na kuhifadhi kumbukumbu zote na nyaraka za kijiji.
• Katibu wa mikutano na kamati zote za Halmashauri ya kijiji.
• Kusimamia utungaji wa sheria ndogo za kijiji.
• Afisa masuhuli na Mtendaji Mkuu na Serikali ya kijiji.
• Kupokea na kusikiliza na kutatua malalamiko na migogoro ya wananchi na
• Kazi nyingine atazopongiwa na mwajiri.
1.2. Sifa Za Mwombaji
• Awe amehitimu elimu ya kidato cha nne au sita pia awe anehitimu mafunzo ya cheti/Astashahada katika moja ya fani, zituatazo:• Utawala, Sheria, Elimu ya Jamii, Usimamizi wa fedha, Maendeleo ya Jamii na Sayansi ya Sanaa kutoka katika chuo chochote kinachotambuliwa na Serikali.
1.3 Ngazi ya Mshahara ni TGS B.
2. KATIBU MAHSUSIHII- Nafasi 01
2.1 Kazi Na Majukumu
• kuchapa barua, taarifa za kawaida.
• Kusaidia kupokea wageni na kuwasaili shida zao na kuwaelekezo sehemu wanapoweza kushughulikiwa.
• Kusaidia kutunza taarifa/kumbukumbu za matukio, miadi, torehe zo vikao. safari za Mkuu wake na ratiba ya kazi nyingine zilizopangwa kutekelezwa katika ofisi anayofanyia kazi na kumuarifu Mkuu wake kwa wakati unaohitajika.
• Kusaidia kufanya na kumpalia Mkuu wake majalada nyaraka au kitu chochote katika shughuli za kazi hapo ofisini.
• Kusaidia kufikisha maelekezo ya Mkuu wake wa kazi kwa wasaidizi wake na pia kuwaarifu kuhusu laarifa zozole anazokuwa anapewa na wasaidizi hao.
• Kusaidia kupokea majalada, kuyagawa kwa maofisa walio katika sehemu alipo na kuyakusanya, kuyatunza na kuyarudisha sehemu zinazohusika na
• Kazi nyingine atazopangiwa na mwajiri.
2.2 Sila Za Mwombaji
• Awe amehitimu kidato cha IV/VI
• Awe amehudhuria mafunzo ya uhaziri na kufaulu mtihani wa hatua ya tatu.
• Awe amefaulu somo la Hati Mkato ya kiswahili na Kiingereza maneno 80 wa dakika moja.
• Awe amepata mafunzo ya Kompyuta kutoka chuo chochote inachotambuliwa na Serikali na kupata cheti katika program za Windows, Microsoft Office, Internet, E-mail na Publisher.
Ngazi ya Mshahara ni TGS B.
3. DEREVA DARAJA II - Nafasi 01
3.1 Kazi Na Majukumu
• Kuendesha Magari ya abiria, na malori,
• uhakiki gari na vyombo vyake vipo katika hali nzuri wakali wote,
• Kufanya uchunguzi wa gari kabla na baado ya safari iii kugunduo ubovu unaohitaji matengenezo.
• Kufanya matengenezo madogo madogo katika gari,
• utunza na kuandika daftari la safari "log-book" kwa 0 safari zote.
• Kazi nyingine atazopangiwa na mwajiri.
3.2 Sifa Za Muombaji
• Awe amehitimu kidato cha IV/VI
• Awe wenye Leseni daraja "C" ya uendeshaji pamoja na uzoefu wa kuendesha magari kwa muda usiopungua miaka mitatu bilo kusababisha ajali
• Awe na cheti cha Majaribio ya Ufundi Daraja la II
• Awe na Cheti kinachotambulika Serikalini
Ngazi ya Mshahara ni TGS B.
3.0 MASHARTI YA JUMLA
i) Waombaji wote wawe ni Raia wa Tanzania.
ii) Waombaji wote wawe na umri kati ya miaka 18-45
iii) Waombaji wote waambatanishe cheti cha kuzaliwa.
iv) Waombaji waambatanishe maelezo binafsi (CV) yenye anuani na namba za simu za kuaminika na majina mawili ya wadhamini.
v) Maombi yaambatishwe na picha moja (Passport size ya hivi karibuni no iandikwe jina kwa nyuma).
vi) Maombi yaambatanishwe no nakala za vyeti vya taaluma/Shule na vyeti vya kuhitimu mafunzo ya vyuo.
vii) Waombaji wote waambatishe na nakala ya kitambulisho cha Taifa (NIDA) - kwa ambao hawana vitambulisho hivyo, namba NIDA ziandikwe kwenye maelezo (CV)
viii) Maombi yote yatumwe kwa njia ya posta kwa kutumia anuani ifuatayo;•
Mkurugenzi Mtendaji,
Halamshauri ya Wilaya,
S.L.P. 160,
KILWA.
Mwisho wa kupokea barua za maombi torehe 13/01/2022 saa 9: 30 Alasiri
NB: Maombi ambayo yatawasilishwa kwa njia ya mkono hayatashughulikiwa.
Pakua Hapa Tangazo hili Rasmi Kutoka Tovuti ya Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa