TANGAZO LA NAFASI ZA AJIRA KWA KADA ZA AFYA NA UALIMU
Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR - TAMISEMI) imepata kibali cha ajira za Watumishi wa Kada mbalimbali za Afya 2,726 kwa ajili ya Hospitali za Halmashauri, Vituo vya Afya na Zahanati pamoja na Walimu 6,949 wa Shule za Msingi na Sekondari watakaofanya kazi chini ya Mamlaka za Serikali za Mitaa nchini.
Kwa sababu hiyo, wahitimu kutoka kwenye Vyuo vya Elimu ya Juu, Vyuo vya Ualimu na Vyuo vya Afya vinavyotambuliwa na Serikali wanatangaziwa kutuma maombi yao ya nafasi za kazi kuanzia tarehe 09 - 23 Mei, 2021. Nafasi za ajira zilizopo ni kwa wahitimu wa Astashahada (Certificate), Stashahada (Diploma) na Shahada (Degree).
Click Here to Join us on Telegram for Instant Job Updates.