Kumb. Na. IMC/S.20/2/VOL.1/12 LNLU5 Tarehe 29/12/2021
TANGAZO LA KAZI
MKURUGENZI WA HALMASHAURI YA MANISPAA YA IRINGA ANAPENDA KUTANGAZA NAFASI ZA KAZI KWA WATANZANIA WOTE WENYE SIFA KAMA
IFUATAVYO: •
1.0 DEREVA DARAJA LA II - (NAFASI 2)
1.1 MAJUKUMU NA KAZI:
i. Kukagua Gari kabla na baada ya safari ili kubaini hali ya usalama wa Gari. ii. Kuwapeleka Watumishi maeneo mbalimbali kwenye safari za kikazi.
iii. Kufanya matengenezo madogo madogo ya Gari. iv. Kukusanya na kusambaza Nyaraka mbalimbali.
v. Kujaza na kutunza taarifa za Safari zote katika daftari la safari (Log book).
vi. Kufanya usafi wa Gari.
vii. Kufanya kazi nyingine kadri utakavyoelekezwa na Msimamizi wako.
1.2 SIFA ZA MWOMBAJI:
Waombaji wawe na Cheti cha Mtihani wa Kidato cha IV wenye Leseni ya Daraja E au Daraja C, ya uendeshaji magari pamoja na uzoefu wa kuendesha magari kwa muda usiopungua Mwaka mmoja bila kusababisha ajali. Awe amehudhuria mafunzo ya msingi ya uendeshaji magari (Basic Driving Course) yanayotolewa na Chuo cha Mafunzo ya ufundi Stadi (VETA) au Chuo kinachotambuliwa na Serikali. Waombaji wenye Cheti cha majaribio ya Ufundi wa Daraja la II watafikiriwa kwanza.
1.3 NGAZI YA MSHAHARA
Ngazi ya Mshahara ni kwa kuzingatia viwango vya serikali yaani TGSB kwa mwezi.
2.0 MSAIDIZI WA KUMBUKUMBU DARAJA LA II - (NAFASI 1)
2.1 MAJUKUMU NA KAZI:
i. Kutafuta kumbukumbu/nyaraka/mafaili yanayohitajiwa na wasomaji.
ii. Kudhibiti upokeaji na uandikishaji wa kumbukumbu/nyaraka.
iii. Kuchambua, kuorodhesha na kupanga kumbukumbu/nyaraka katika makundi kulingana na somo husika (Classification and Boxing) kwa ajili ya matumizi ya ofisi.
iv. Kuweka/kupanga kumbukumbu/nyaraka katika reki (file rakes/cabinets)
katika Masijala/Nyumba vya kuhifadhia kumbukumbu.
v. Kuweka kumbukumbu (barua, nyaraka nk) katika mafaili.
vi. Kushughulikia maombi ya kumbukumbu/nyaraka kutoka Taasisi za Serikali.
2.2 SIFA ZA WAOMBAJI
Waombaji wawe wamehitimu Kidato cha nne au cha Sita, wenye cheti cha Utunzaji
Kumbukumbu katika mojawapo ya fani za Afya, Masijala, Mahakama na Ardhi.
2.3 NGAZI YA MSHAHARA
Ngazi ya Mshahara ni kwa kuzingatia viwango vya serikali yaani TGSB kwa mwezi.
3.0 MTENDAJI WA MTAA DARAJA LA III - (NAFASI 2)
3.1 MAJUKUMU NA KAZI
i. Katibu wa Kamati ya Mtaa. ii. Mtendaji Mkuu wa Mtaa.
iii. Mratibu wa utekelezaji wa Sera na Sheria zinazotekelezwa na Halmashauri katika
Mtaa.
iv. Mshauri wa Kamati ya Mtaa kuhusu mipango ya maendeleo katika Mtaa.
v. Msimamizi wa utekelezaji wa Sheria ndogo pamoja na Sheria nyingine zinazotumika katika Mtaa.
vi. Mshauri wa kamati ya Mtaa kuhusu masuala ya ulinzi na usalama.
vii. Msimamizi wa utekelezaji wa mikakati mbalimbali inayohusu uondoaji wa njaa na umaskini katika Mtaa.
viii. Kusimamia ukusanyaji wa mapato ya Halmashauri na kutunza kumbukumbu za walipa kodi wote.
ix. Kuandaa na kutunza rejesta ya wakazi wote wa Mtaa.
x. Atawajibika kwa Mtendaji wa Kata.
3.2 SIFA ZA WAOMBAJI
Waombaji wawe wamehitimu kidato cha nne (IV) au sita (VI). Waliohitimu mafunzo ya Astashahada katika moja ya fani zifuatazo; Utawala, Sheria, Elimu ya Jamii, Usimamizi wa Fedha, Maendeleo ya Jamii na Sayansi ya Sanaa kutoka Chuo cha Serikali za Mitaa Hombolo, Dodoma au Chuo chochote kinachotambuliwa na Serikali.
3.3 NGAZI YA MSHAHARA
Ngazi ya Mshahara ni kwa kuzingatia viwango vya serikali yaani TGSB kwa mwezi.
MASHARTI YA UJUMLA
i. Mwombaji lazima awe raia wa Tanzania na awe tayari kufanya kazi katika Idara yoyote atakayopangiwa.
ii, Mwombaji awe na umri usiopungua miaka 18 na usiozidi miaka 45.
iii. Mwombaji aambatishe maelezo yake binafsi yanayojitosheleza (Detailed CV)
yenye anuani na namba za simu za kuaminika.
iv. Mwombaji aambatishe nakala ya vyeti vya uendeshaji magari (Taaluma), cheti cha Kidato cha IV, Cheti cha Kuzaliwa na picha mbili za rangi za hivi karibuni na ziandikwe majina kwa nyuma, nakala hizo zithibitishwe na Hakimu au Wakili.
v. Mwisho wa kupokea barua za maombi ni tarehe 11 Januari, 2022 Saa 9:30 Alasiri.
Maombi yote yatumwe kupitia anuani ya posta kama ifuatavyo;•
Mkurugenzi wa Manispaa,
Halmashauri ya Manispaa ya Iringa,
S.LP. 162,
IRINGA.
NB: Tangazo hili linapatikana pia kwenye Tovuti ya Halimashauri ya Manispaa ya Iringa ambayo ni www.iringamc.go.tz
Bofya hapa ili kuwownload Tangazo Hili Katika Mtindo Rahisi Kuprint wa PDF