Taasisi ya Kuzuia na Kupamabana na Rushwa (TAKUKURU) ni taasisi ya Umma iliyoanzishwa chini ya Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Namba 11 ya Mwaka 2007. Sheria hii ilitungwa baada ya kufutwa kwa Sheria ya Kuzuia Rushwa (TAKURU) Sura ya 329 iliyofanyiwa marrejeo mwaka 2002. Kuanzishwa kwa chombo hiki kulikuja baada ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitisha Mswaada wa Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa wa mwaka 2007 mnamo tarehe 16 Aprili, 2007. Mswaada huu ulisainiwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Jakaya Kikwete kuwa Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa mnamo tarehe 11Juni, 2007 na ilianza kufanya kazi tarehe 1Julai, 2007.
TANGAZO LA MTIHANI WA USAILI
Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) anapenda kuwatangazia watu wote walioomba nafasi ya ajira ndani ya Taasisi ya kuzuia na Kupambana na Rushwa kwamba mtihani wa usaili wa maandishi (apptitude test) utafanyika Jijini Dodoma siku ya tarehe 8.1.2022.
Mambo Muhimu ya Kuzingatia
1. Tarehe ya usaili ni tarehe 8.1.2022 siku ya Jumamosi;
2. Kwa waombaji ambao wameomba kazi ya Afisa Uchunguzi mtihani wao utaanza saa 2:30 asubuhi siku hiyo tarehe 8.1.2022;
3. Kwa waombaji ambao wameomba nafasi ya Uchunguzi Msaidizi mtihani wao utaanza saa 6:00 mchana siku hiyo ya tarehe 8.1.2022;
4. Waombaji walioitwa kwenye usaili huu wahakikishe wanachukua tahadhari
zote za kujikinga na ugonjwa wa UVIKO-19 muda wote wanaposafiri na wanapokuwa kwenye chumba cha mtihani;
5. Majina ya waombaji wote walioitwa kwenye usaili pamoja na eneo la
kufanyia mtihani yanapatikana kwenye wavuti ya TAKUKURU
wwww.pccb.go.tz;
6. Kila mwombaji ajaze taarifa zake binafsi kwenye fomu ambayo imeambatishwa na orodha ya majina. Fomu pia inapatikana kwenye wavuti ya TAKUKURU pccb.go.tz:
7. Fomu ya taarifa binafsi ijazwe kwa umakini na kwa usahihi. Fomu hiyo ni
sehemu ya mtihani wa apptitude test, kwa hiyo mtu atakayejaza vibaya Fomu hiyo atakuwa ameipoteza nafasi ya kufaulu kwenye usaili huu;
8. Fomu hivo iwasilishwe siku ya mtihani tarehe 8.1.2022. Msailiwa ambaye
hatawwasilisha_Fomu_hio atahesghikakuwanimiongonimwa walioshindwg kwenve usaili.
9, Watakaofaulu kwenye mtihani wa maandishi ndio watakaoitwa kwenye usaili wa mahojiano (oral interview)
Imetolewa na
Mkurugenzi Mkuu,
Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa, Mtaa wa Jamhuri,S
S.L.P 1291,
41101 DODOMA.
IMPORTANT INTERVIEW DOCUMENTS FROM PCCB:-
MPANGILIO WA WASAILIWA KATIKA VITUO
ORODHA YA WALIOITWA KWENYE USAILI KWA MAAFISA UCHUNGUZI