TANGAZO LA NAFASI ZA AJIRA ZA KONSTEBO WA UHAMIAJI (470)
Kamishna Jenerali wa Uhamiaji anatangaza nafasi za ajira za Konstebo wa Uhamiaji 470 (Wenye Shahada ya Kwanza nafasi 70, Kidato cha Sita nafasi 100 na Kidato cha Nne nafasi 300).
Waombajj wawe wamefuzu mafunzo mbalimbali ya Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) au Jeshi la Kujenga Uchumi (JKU) waliopo Makambini au nje ya kambi wenye sifa zifuatazo:-
1. SIFA ZA WAOMBAJI
i. Awe raia wa Tanzania;
ii. Awe na Cheti cha Kuzaliwa (Birth Cetificate);
ii. Awe na Kitambulisho au Namba ya Kitambulisho cha Taifa (NIDA);
iv. Awe na vyeti vya kuhitimu shule (Leaving Certificates), vyeti vya taaluma
(Academic Certificate) na cheti cha kuhitimu mafunzo ya awali ya JKT/JKU katika oparesheni mbalimbali;
v. Awe na afya njema ya mwili na akili,
vi. Awe na tabia njema, asiwe amewahi kufungwa, kujihusisha na matumizi au biashara ya dawa za kulevya, au uhalifu wa aina yoyote;
vii. Asiwe na alama yoyote au michoro katika mwili wake;
viii. Asiwe ameoa au kuolewa;
ix. Awe tayari kuhudhuria mafunzo ya awali ya Uhamiaji;
x. Awe tayari kufanya kazi mahali popote nchini Tanzania;
xi. Baada ya kuajiriwa atafanya kazi kwa muda wa miaka minne (4) bila kuoa au kuolewa;
xii. Waombaji wenye Shahada ya Kwanza wawe na umri usiozidi miaka 30; awe amehitimu mafunzo katika moja ya fani zifuatazo:- Uhandisi Ujenzi (Civil Engineering), Umeme (Electrical Engeneering), Mkadiriaji Majenzi (0S), Msanifu Majengo (Architect), Afisa Tabibu, Tabibu Msaidizi, Uuguzi, Takwimu, Masuala wa Bima, Msanifu Mifumo ya Kielekroniki (System Developer), Usalama wa Mtandao (Cyber Security), Usalama wa Mifumo (Information Security), Wataalam wa Lugha (Kiarabu, Kichina, Kifaransa, Kirusi, Kihispaniola, Kitaliano, Kireno), Wakalimani (Translators) na Mtaalam wa Lugha za alama;
xiii. Waombaji wa Kidato cha Sita na Nne wawe na umri usiopungua miaka 18 na usiozidi miaka 28.
Aidha, waombaji hao wawe na Cheti cha Taaluma kutoka katika Vyuo mbalimbali vinavyotambuliwa na serikali katika fani zifuatazo:• Umeme, Ushonaji, Ufundi wa Magari, Fundi Bomba, Uashi, Fundi Uchomeleaji, Seremala, Taaluma za Uuguzi, Mtunza kumbukumbu za Ofisi, Katibu Muhtasi, Tabibu, Maabara, Udereva, Michezo, Muziki, Uimbaji, Uhandisi wa Sauti (Sound Engineering), Mpiga Vyombo vya Muziki, Upishi,Ugani pamoja na Fundi wa Viyoyozi (AC) - magari au nyumba, watapewa kipaumbele
2. NAMNA YA KUTUMA MAOMBI:
Mwombaji anatakiwa kuandika barua ya Maombi ya ajira kwa mkono wake akiambatisha nyaraka zifuatazo:•
i. Barua ya Utambulisho toka Serikali ya Mtaa/Kijiji au Shehia;
ii. Waombaji waliopo Makambini, barua zao zipitie kwa Wakuu wa Kambi husika;
iii. Nakala ya Cheti cha Kuzaliwa;
iv. Nakala Kitambulisho cha Taifa (NIDA) au namba ya Kitambulisho cha Taifa au Kitambulisho cha Mzanzibari;
v. Nakala ya vyeti vya kuhitimu shule (Leaving Certificates);
vi. Nakala ya vyeti vya Taaluma (Academic Certificates);
vii. Nakala ya vyeti vingine vya Fani mbalimbali;
viii. Wasifu wa Mwombaji (CV); na
ix. Picha Nne (04) (Passport size) zenye rangi ya bluu bahari.
3. MAOMBI YA AJIRA YATUMWE KWA ANUANI ZIFUATAZO:
a) Waombaji waliopo Tanzania Bara watume maombi yao kwa;
KAMISHNA JENERALI WA UHAMIAJI,
4 BARABARA YA MWANGOSI,
UZUNGUNI, S. L. P. 1181, DODOMA.
b) Waombaji walioko Zanzibar watume maombi yao kwa;
KAMISHNA WA UHAMIAJI,
AFISI KUU, S.LP. 1354, ZANZIBAR.
4. Mwisho wa kupokea maombi ya ajira ni tarehe 14 Januari, 2022.
5. Tahadhari;
Ikumbukwe kuwa Mwombaji yoyote atakayebainika kuwasilisha nyaraka za kughushi atachukuliwa hatua za kisheria ikiwa ni pamoja na kufikishwa Mahakamani.
BOFYA HAPA ILI KUPAKUWA TANGAZO HILI RASMI KATIKA MFUMO WA PDF
TAP OR CLICK HERE TO DOWNLOAD THE OFFICIAL ANNOUNCEMENT IN PDF FORMAT
The Deadline for Receiving Applications is 14th January 2022.
Also View: Other Government Jobs Here
See More Immigration Jobs Here