TANGAZO LA NAFASI  YA KAZI Mkurugenzi   Mtendaji   Halmashauri   ya  Wilaya   ya  Muleba  anapenda   kuwatangazia wananchi wote nafasi za kazi ya ajira ya Mtendaji wa kijiji  Ill  nafasi moja (1)


TANGAZO LA NAFASI  YA KAZI

Mkurugenzi   Mtendaji   Halmashauri   ya  Wilaya   ya  Muleba  anapenda   kuwatangazia wananchi wote nafasi za kazi ya ajira ya Mtendaji wa kijiji  Ill  nafasi moja (1)


1.JINA LA KAZI MTENDAJI WA KIJIJI Ill  (NAFASI 1) 

A.  MAJUKUMU

1.              Afisa Masuhuli  na Mtendaji Mkuu wa Serikali ya Kijiji

ii.      Kusimamia  Ulinzi  na Usalama wa Raia na Mali zao,  kuwa mlinzi  wa amani  na Msimamizi wa Utawala Bora katika Kijiji.

iii.      Kuratibu  na kusimamia  upangaji  wa utekelezaji  wa Mipango ya Maendeleo  ya Kijiji

iv.      Katibu wa Mikutano na Kamati zote za Halmashauri ya kijiji

v.      Kutafsiri   na kusimamia sera, sheria na taratibu

vi.      Kuandaa  taarifa  za  utekelezaji  wa  kazi  katika  eneo  lake  na  kuhamasisha wananchi katika kuandaa na kutekeleza mikakati ya kuondoa njaa, umaskini na kuongeza uzalishaji mali

vii.      Kiongozi Mkuu wa vitengo vya kitaalamu katika kijiji

viii.      Kusimamia,  kukusanya na kuhifadhi kumbukumbu zote na nyaraka zote

ix.      Mwenyekiti wa kikao cha Wataalamu waliopo katika kijiji
x.      Kupokea,  kusikiliza na kutatua malalamiko ya wananchi

xi.      Kusimamia utungaji wa sheria ndogo za kijiji  na

xii.      Atawajibika kwa Mtendaji wa Kata.


Dont Miss Out: Get All the New Job Updates Here 

 
B.  SIFA ZA MWOMBAJI
i.        Awe na Elimu ya kidato cha nne na kuendelea
ii.       Awe  amehitimu  masomo Astashahada/Cheti  katika  fani  ya  Utawala,
Sheria,  Elimu ya Jamii,  Usimamizi wa Fedha,  Maendeleo ya jamii na Sayansi  ya  Sanaa  kutoka  Chuo  cha  Serikali  za  Mitaa  Hombolo Dodoma, au Chuo chochote kinachotambuliwa na Serikali.


C.  NGAZI YA MSHAHARA TGS B

D.  UTARATIBU WA KUTUMA MAOMBI YA NAFASI ZA KAZI
i.        Barua za maombi ziandikwe kwa mkono
ii.       Barua za maombi ya nafasi za kazi ziandikwe kwa:•

MKURUGENZI  MTENDAJI (W), HALMASHAURI YA WILAYA, S.L.P 131,
MULEBA.

iii.      MWOMBAJI AAMBATANISHE:

•   Curriculum Vitae (CV) yenye anuani na namba za simu za kuaminika pamoja na majina  ya wadhamini  (Referees) watatu wa kuaminika
•    Nakala za vyeti vya Elimu ya Sekondari  na Chuo
•    Hati ya kuzaliwa (Birth Certificate)
•    Picha moja ya "PASSPORT SIZE" ya hivi  karibuni
•    Nakala ya Kitambulisho cha Taifa  (NIDA)

Dont Miss Out: Get All the New Job Updates Here


iv.       MAMBO MUHIMU YA KUZINGATIA
•    Waombaji  wote  wawe  ni   Raia wa  Tanzania  na wenye  umri usiozidi miaka 45
•    Barua    za    uthibitisho/matokeo    ya    mitihani    (Testimonals/
provisional/ statements of result hazitapokelewa
•    Waombaji waliosoma  nje ya Tanzania wahakikishe vyeti vyao vimehakikiwa na kuidhinishwa na Mamlaka husika (NACTE na NECTA)
•  Waombaji   waliostafishwa   katika   Utumishi   wa   Umma hawaruhusiwi  kuomba .isipokwa  kama wana  kibali  cha Katibu Mkuu Kiongozi
•  Uwasilishaji  na taaarifa  na sifa  za  kugushi  wahusika watachukuliwa hatua za kisheria


MWISHO WA KUPOKEA MAOMBI YA NAFASI ZA KAZI  NI TAREHE 04/02/2022



WOTE WENYE SIFA WANAKARIBISHWA


IMETOLEWA NA OFISI YA, MKURUGENZI  MTENDAJI, HALMASHAURI YA WILAYA YA MULEBA.

Dont Miss Out: Get All the New Job Updates Here

 Also See: Other Government Jobs Here

See Also : Other Jobs in Kagera Region Here