YAH: TANGAZO LA NAFASI YA KAZI
Halmashauri ya Wilaya ya Maswa kupitia kibali cha ajira mbadala Kumb. Na.FA.170/533/01"8"/65 cha tarehe 26 Novemba 2021, kilichotolewa na Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora inatangaza nafasi wazi moja [1] ya Mtendaji wa kijiji Daraja la Ill na Dereva Daraja la II.
1.0 MTENDAJI WA KIJIJI DARAJA LA II - NAFASI 1
1.1. Sifa za Mwombaji:-
• Wahitimu wa kidato cha nne au sita wenye cheti cha [NTA Level 5] au
Certificate katika moja ya fani zifuatazo.
• Utawala
• Usimamizi wa Rasilimali watu
• Maendeleo ya Jamii au
• Sayansi ya Jamii kutoka Chuo cha Serikali za Mitaa Hombolo, Dodoma au chuo chochote kinachotambuliwa no Serikali
(iii) Awe no umri usiozidi miaka 45 (iv) Awe no cheti cha kuzaliwa.
1.2. MAJUKUMU YA KAZI
(i) Afisa Masuuli na Mtendaji Mkuu wa Serikali ya kij,
(ii) Kusimamia Ulinzi no Usalama wa Raia no Mali zoo, kuwa mlinzi wa Amani no Msimamizi wa Utawala bora katika kijiji.
(iii) Kuratibu na kusimamia upangaji wa utekelezaji wa Mipango ya
Maendeleo ya Kijiji.
(iv) Katibu wa Mikutano no Kamati zote za Halmashauri ya Kijiji. (v) Kutafasiri na kusimamia Sera, Sheria no Taratibu.
(vi) Kuandaa taarifa za Utekelezaji wa kazi katika eneo lake no kuhamasisha wananchi katika kuandaa no kutekeleza mikakati ya kuondoa njaa, umaskini no kuongeza uzalishaji Mali.
(vi) Kiongozi wa Wakuu wa vitengo vya Kitaalam katika Kijiji.
(viii) Kusimamia, kukusanya na kuhifadhi kumbukumbu zote no nyaraka za
Kijiji.
(ix) Mwenyekiti wa kikao cha Wataalamu waliopo katika Kijiji.
(x) Kupokea, kusikiliza na kutatua malalamiko na Migogoro ya Wananchi. (xi) Kusimamia utungaji wa Sheria ndogo za Kijiji.
(xii) Atawajibika kwa Mtendaji wa Kata.
(xiii) Kazi nyingine utakayopewa no Mkuregenzi Mtendaji wa Halmashauri.
1.3 NGAZI YA MSHAHARA
Mshahara: Ngazi ya TGS 8 kwa mwezi.
2.0 DEREVA DARAJA LA II - NAFASI 1
2.1 SIFA ZA MWOMBAJI
(i) Awe no elimu ya kidato cha IV au VI (ii) Awe no leseni daraja la "C"
(iii) Awe no uzoefu wa kuendesha magari kwa muda usiopungua miaka mitatu bila kusababisha ajali
(iv) Awe no umri usiozidi miaka 45
(v) Awe no cheti cha Majaribio ya Ufundi Daraja la II (vi) Awe na cheti cha kuzaliwa
2.2 MAJUKUMU YA KAZI
(i) Kukagua gari kabla no baada ya safari iii kubaini hali ya usalma wa gari
(ii) kuwapeleka watumishi maeneo mbalimbali kwenye safari za kikazi
(iii) kufanya matengenezo madogo madogo ya gari
(iv) kukusanya no kusambaza nyaraka mbalimbali
(v) kujaza no kutunza taarifa za safari zote katika daftari la safari
(vi) kufanya usafi wa gari
(vii) kufanya kazi nyingine kadri atakavyoelekezwa na msimamizi wake
2.3. NGAZI YA MSHAHARA
Mshahara: Ngazi ya TGS 8 kwa mwezi.
3.0. MASHARTI YA JUMLA
• Awe raia wa Tanzania.
• Awe na umri wa kuanzia miaka 18 hadi 45
• Waombaji waambatanishe na nakala za cheti cha kuzaliwa, vyeti vya kuhitimu mafunzo na vyeti vya kidato cha nne vilivyodhibitishwa na Wakili au Mahakama.
• Muombaji ambatanishe picha mbili [2] ndogo ya rangi [passport size] ya hivi karibuni
• Testimonials, Provisional results, Statement of results na hati za matokeo ya kidatocha nne na sita [form VI and form IV result slip] HAVITAKUBALIWA.
• Waombaji waliostaafishwa katika Utumishi wa Umma hawaruhusiwi kuomba isipokuwa kwa Kibali cha Katibu Mkuu Kiongozi.
4.0. UTARATIBU WA KUTUMA MAOMBI
Maombi yote yatumwe kwa:•
Mkurugenzi Mtendaji (W), Halmashauri ya wilaya ya Maswa, S.L.P. 170,
MASWA -SIMIYU.
Mwisho wa kupokea maombi ni tarehe 18.01.2021 Saa 9.30 alasiri.
NB:
Tangazo hili linapatikana katika Tovuti ya Halmashauri www .maswadc.go.tz Tovuti ya Sekretarieti ya Ajira www .ajira.go.tz na katika mbao za matangazo za Halmashauri na Mkoa wa Simiyu.
Pakua Hapa Tangazo hili Rasmi Kutoka Tovuti ya Halmshauri ya Wilaya ya Maswa